UTANGULIZI

Unapotaka kuhost website ndogo, uchaguzi wa hosting ni rahisi kwani shared hosting itakupa vitu vyote utakazozihitaji kwa bei rahisi. Lakini website yako inavyozidi kuwa maarufu na kuwana functions nyingi ugomvi na shared hosting server unakuwa mkubwa na suluhisho pekee ni kuhamia kwenye server zenye kutoa ubora zaidi kwenye rasilimali za server. Hosting hizo zinaitwa VPS, Semi Dedicated na Dedicated servers. Zote tatu zinakupa IP address ya kwako mwenyewe na server ya kwako mwenye.

Fuatilia tofauti zao hapa chini

  1. Semi Dedicated server (Hii huduma unasimamiwa na data center administrators kama ilivyo kwenye shared hosting. unakuwa na server yako mwenyewe hivyo ukipatwa na tataizo ni wewe mwenyewe. bei ni kuanzia elfu 80 kwa mwezi na kuendelea)
  2. VPS (Hii huduma ni kama hapo juu ila wewe mwenyewe ndio unasimamia server. unakuwa na server yako mwenyewe hivyo ukipatwa na tataizo ni wewe mwenyewe. bei ni kuanzia elfu 80 kwa mwezi na kuendelea)
  3. Dedicated server (Hii huduma ni kama hapo juu ila wewe unamiliki device yote mwenyewe na mwenyewe ndio unasimamia server. unakuwa na device yako mwenyewe na server yako mwenyewe hivyo ukipatwa na tataizo ni wewe mwenyewe. bei ni kuanzia laki 3 kwa mwezi na kuendelea)
Kwa website zinazotembelewa sana na zinafuntion muhimu zenye kuhitaji umakini wa server, VPS ni nzuri au Semi dedicated server. Chagua VPS kama una mtaalamu wa kusimamia au chagua semi dedicated kama huna mtaalamu kwani semi dedicated server inakupa functions zote na service itasimamiwa na data center administrators kwa niaba yako.
Kama biashara yako inatunza nyaraka muhimu za wateja kama credit cards na akaunti za fedha ahasa kwa mabenki na taasisi za malipo online, tafadhali chagua dedicated server ili uwe na umiliki wa server kwa asilimia 100.

Pin It on Pinterest

Share This