Vitu vinavyotakiwa ili kutengeneza website ya kampuni ya utalii ni hivi hapa chini:

#1.  Unatakiwa uwe na domain au jina linaloakisi biashara ya utalii

Mfano

  • safariforleisure.com
  • safariforleisure.co.tz
  • wildlifeadventure.com
  • wildlifeadventure.co.tz
  • hakunamatatatours.com
  • hakunamatatatours.co.tz

#2.  Unatakiwa pia kununua hosting

Maelezo kuhusu hosting na tofauti zao

Kwa matumizi madogo tunashauri shared hosting na kwa matumizi makubwa na muhimu tunashauri VPS yaani Virtual Private Server na kwa yale matumizi maalumu yenye kuihitaji usalama wa hali ya juu tunashauri dedicated server.  Shared server ni rahisi sana kwani zinakuwa kati ya dola moja hadi dola 10 kwa mwezi  wakati, VPS inakupatia vionjo vyote vya dedicated server kwa bei ya wastani kati ya dola 10 hadi chini ya mia kwa mwezi. Dedicated server senyewe bei zake ziko juu kwani zingine zaweza fika dola mia na zaidi kwa mwezi

#3.  Taarifa za website

Ukishanunua hosting unatakiwa kuanda taarifa za kuweka kwenye website kwa mfumo huu hapa chini. Kumbuka taarifa ni pamoja na maneno, sauti, video na picha.

Tuwasiliane kwa maelezo na huduma bora