Vitu vinavyotakiwa ili kutengeneza website ya kanisa ni hivi hapa chini:

#1.  Unatakiwa uwe na domain au jina linaloakisi jina la Kanisa

Mfano

  • kristomfalme.church
  • kristomfalme.or.tz
  • kristomfalmechurch.or.tz

#2.  Unatakiwa pia kununua hosting

Maelezo kuhusu hosting na tofauti zao

Kwa matumizi madogo tunashauri shared hosting na kwa matumizi makubwa na muhimu tunashauri VPS yaani Virtual Private Server na kwa yale matumizi maalum yenye kuhitaji usalama wa hali ya juu tunashauri dedicated server.  Shared server ni rahisi sana kwani zinakuwa kati ya dola moja hadi dola 10 kwa mwezi  wakati, VPS inakupatia vionjo vyote vya dedicated server kwa bei ya wastani kati ya dola 10 hadi chini ya mia kwa mwezi. Dedicated server senyewe bei zake ziko juu kwani zingine zaweza fika dola mia na zaidi kwa mwezi

#3.  Taarifa za website

Ukishanunua hosting unatakiwa kuanda taarifa za kuweka kwenye website kwa mfumo huu hapa chini. Kumbuka taarifa ni pamoja na maneno, sauti, video na picha

 Mpangilio na muundo pendekezwa wa website

KUHUSU KANISA

  • Uongozi wa Kanisa
  • Barua ya Mchungaji Kiongozi
  • Historia ya Kanisa
  • Maono na Utume
  • Tunu za Kanisa
  • Tamko la Imani

HUDUMA ZA KANISA

  • Idara ya Watoto
  • Ibada za Kanisa
  • Kwaya
  • Vijana –
  • Akina Mama – WWK
  • Uinjilisti na Umisheni
  • Wajane na Yatima
  • Makanisa ya Maeneo

MIRADI YA KANISA

  • Mradi wa Akina Mama
  • Mradi wa Ujenzi wa Kanisa
  • Mradi wa shule
  • Academy
  • Mradi wa Kwaya
  • Mradi wa Compassion

HABARI NA MATUKIO

  • Matukio Juma Hili
  • Habari Picha (Picha za matukio zipangwe kulingana na matukio)
  • Kalenda ya Kanisa ya mwaka (Matukio ya kuweka kwenye website kwa mwaka mzima)
  • Ratiba ya wiki

SHUHUDA NA MAONI

MAWASILIANO

  • Jina ya Idara/kitengo
  • Jina la mkuu wa kitengo/idara
  • Simu
  • EMail
  • Ramani ya Google

HUDUMA ZA KICHUNGAJI

  • Jina la mchungaji au mtumishi
  • Simu ya mkononi

MAHITAJI NA MAOMBEZI